Rasilimali Zinazoaminika Minyororo salama, inayoweza kufuatiliwa na ya dijitali kwa bidhaa zako.

Wasiliana nasi

Inayotuhusu

Katika kutazamiya mpito wa nishati ilio muhimu kiuchumi, kiikolojia (kimazingira) na kisiasa na kwa ngazi ya umma pia, kumeazishwa teknolojia mpya za uzalishaji wa nishati na kupunguza utowaji wa dioksidi ya kaboni. Kwa kutekeleza kiufundi mpito huu wa nishati, ni muhimu kuwa na malighafi ao madini zisizokuwa za migogoro (Mizozo).

Uzalishaji wa malighafi na madini muhimu nyingi inaambatanishwa na inchi zinazokosa usalama na zenye migogoro. Kwa hiyo, uchuhuzi wa bidhaa iyi umewekewa azimio kali za kisheria. Hata hivyo, utekelezaji wa sheria hizo unaleta mazara kwa rahiya wengi ambao wanategemeya zaidi uchimbaji wa madini kwa mikono ao kwa kutumiya vyombo vidogo vidogo (ASM). Utekelezaji wa azimio hizo unatatiza uwekezaji kiuchumi, na hivyo inaleta ugumu kwa uchimbaji wa kudumu wa madini na uchuhuzi wake. Iyi inasabisha uchunguzi wa sekta ya uchimabaji madini kwa vyombo vidogo vidogo kuwa ngumu.

IotaOrigin UG inashugulika na iyi maswala muhimu ya kiuchumi na ya kijamii yaliyotajwa hapo juu. Iyi ni pamoja na uchimbaji wa madini kwa kuheshimu haki zakibinadamu na mazingira, na kufuatiliya muongozo wa OECD juu ya kanuni za usawa wa uchukuzaji wa madini, lakini piya kwa kutekeleza sheria zakimataifa usika. Lengo la IotaOrigin UG si kuhakikisha mabadiliko ya nishati yanayokubalika tu, lakini pia kutimiza Malengo ya Maendeleo Yakudumu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kwa kusaidia warahia wa maeneo kunako chimbwa madini.

Huduma

Ni nini umaalumu wa ofa yetu?

IotaOrigin ni jukwaa la kimataifa yakufanya biashara ya madini na bidhaa visiyokuwa na mizozo. Kwa kuongezea, IotaOrigin inawezesha kufuatiliya madini zisizokuwa na mizozo kupitiya programu za teknolojia inayo kubalika kwenye mitandao yakisasa. Hii uwezesha wahusika wote kwenye mnyororo wa ugavi wa bidhaa kutii muongozo wa kanuni za OECD juu ya madini inayotoka kwa maeneo za mizozo na zenye hatari kubwa, huku zikichungwa vizuri siri za mikataba ya biashara kati ya wausika.

Faida

Unaweza kufaidika na nini?

  • Kufuatilia kidijitali na bila malipo madini zisizokuwa na mizozo, na uwezekanao wa kuboresha uchumi na mapato kibiashara kupitiya data zinazoifaziwa ndani ya minyororo ya ugavi wa bidhaa;
  • Kufuatilia madini zisizokuwa na mizozo kwa heshima ya mikataba ya uchuhuzi, na kurahisisha uwepo wa soko huru na bei nzuri kuliko soko za aina yakujifunga;
  • Kuzingatia kanuni za kimataifa;
  • Kuraisisha ugavi ulio sawa na wakudumu na vilevile uchuhuzi wa madini zisizokuwa na mizozo.

Lengo

Safari ya kwenda.

Ugavi wakudumu na wa heshima ni kipengele muhimu kwa kutimiza malengo ya maendeleo yakudumu ya Umoja wa mataifa. Kupitiya jitihada zake, IotaOrigin UG inakusudia kuchangiza kwa utekelezaji wa malengo hayo na kufanya hatua yakuzamirisha watu wakati wakununua madini, ili rahiya wa maeneo husika wapate sapoti ao faida kutoka kazi za madini.

FAQs

Hesabu ya watu wanaotumika kazi katika sekta ya uchimbaji madini madogo madogo imezidishwa kwa mara tatu tangu mwaka 1993 na kufikia kiwango inayokaribia watu milioni 45. Kunajiongeza hesabu ya watu takribani milioni 60 kwa 150 wanaotegemea mazao ya sekta ya uchimbaji madini madogo madogo. Takribani 90% ya wachimba zahabu wanapatikana katika sekta ya ASM (madini madogo madogo) na wanachangiza angalao 20% ya mapato ya zahabu kila mwaka duniani. Sekta iyi ya ASM ikinyoroshwa ipasavyo, inawezachangiza kwa utekelezaji wa malengo ya umoja wa mataifa (SDGs).

Kuifanya rasmi sekta ya uchimaji madini madogo madogo, ambayo sio rasmi kwa wakati huu kwa ngazi kubwa, inaweza changiza kwa kuzitekeleza malengo zifuatazo : kazi ilio sahii na ukuzi wa uchumi wa kudumu, afya na usawa wa maisha, kushirikiana kwa kufikia malengo ya maendelo yakudumu, ukingo wa maisha ndani ya maji na kwenye udongo, na usawa kijinsia (wanawake na wanaume).

Malengo ya maendeleo yakudumu (SGDs) inafungwa katika malengo 17 kwa ajili ya maendelo ya ujio ulio wa kudumu. SDGs zilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mu mwaka 2015 na zinapaswa kufikiwa munamo mwaka wa 2030. Kwa mujibu wa kitengo cha maendeleo cha umoja wa mataifa (UNDP), sekta ya uchimabaji madini madogo madogo inaweza changiza kwa kiasi kikubwa kufikia malengo hayo. Ikiwemo kupunguza umaskini, elimu, miji na jamii zinazostawi, nishati zakubadilishwa, ubunifu na miundombinu.

Madini muhimu inamaanisha madini ilio muhimu kwa maendeleo yakudumu na kwa upanuzi wa teknolojia za kisasa. Vilevile ziko muhimu kiuchumi na kwa mikakati, lakini ugavi wao ulio salama ahuja akikishwa. Umoja wa Ulaya hutowa ripoti baada ya kila miaka mitatu ambayo inahorozesha kwa sasa ahina 30 za madini muhimu zinazochimbwa kwa sehemu kubwa katika sekta ya uchimbaji madini madogomadogo.

Kulingana na OECD, madini ya migogoro ao ya mizozo ni madini ambayo inawezasababisha kutokeya kwa migogoro, kuikuza ao kuirefusha. Kwa hiyo, utawala na sheria za inchi huzoofika, upungufu wa amani na unyanyasaji mkubwa wa haki zakibinandamu huongezeka. Madini ya mizozo zinawezaharibu usalama mdogo ambao unaonekana katika inchi za hatari kubwa na ambamo vitengo vya kiserekali ni vizaifu. Hii ndiyo sababu OECD imepana muongozo kuhusu uangalifu unaopaswa kuzingatiwa wakati wa kununua madini kama vile bati, tantalum, tungsten na dhahabu (ambayo inaitwa tena 3TG = Tin, Tantalum, Tungsten na Gold) katika maeneo yenye hatari kubwa. Zikilingana na miongozo ya OECD iliyokubaliwa na jumuiya ya kimataifa, sheria ya Umoja wa Ulaya kuhusu madini ya migogoro au sheria ya Dodd-Frank ya Marekani (Sek. 1502) nazo zikakubalika.

Kwa jukwaa letu la "Hideless" [Isiyofichwa], tunataka kuleta uvumbuzi wa kidijitali kwa kiwanda ya madini ambayo hapo awali haikuwa ya dijitali. DLT inatupa mazingira bora ya kutekeleza usalama ulio sahii, uadilifu na uwazi wakurizisha. IotaOrigin inafanya kazi ya kusawazisha na kuweka kidijitali biashara, fedha, bima (assurence) na mikataba ya kimataifa katika sekta ya madini. DLT na kwa upekee IOTA hutupatia vyombo bora zaidi za kukamilisha kazi zetu.

Kwa IotaOrigin, tunatumia usimbaji fiche kutoka mwanzo hadi mwisho ili kuhakikisha ulinzi wa hati za watumiaji huku tukiwezesha ubadilishanaji wa taarifa kati ya wausika katika minyororo ya usambazaji bidhaa. Kupitia mtandao wa IOTA tunaweza kuhakikisha usalama na uadilifu wa data na hati zinazobadilishwa ndani ya mtandao. IotaOrigin haina ufikiaji ao uthibiti wa data iliyobadilishwa kati ya washiriki wake. Hii inakuwezesha kuzingatia kanuni za kimataifa bila kufichua siri za biashara.

Unaweza kushiriki ao kuchangiza kwa mafanikio ya IotaOrigin kwa kugawa maono yake na wengine. Unaweza pia kuwasiliana nasi hapa kwa mahitaji mengine yoyote.

Sarafu ao vikoroti vinavyolingana na teknolojia ya kriptografia ni uvumbuzi muhimu katika malipo ya kimataifa. Inapunguza ada katika biashara ya kimataifa na kufupisha mda wakutuma pesa. IotaOrigin inafanya kazi pia kwa kupata suluhisho zinazoweza kurahisisha na za uwazi katika biashara ya kimataifa ya madini na inaunga mkono malengo ya mpango wa uwazi wa sekta ya uziduaji ao uchimbaji (EITI).

Habari mpya zaidi